Polisi yakamata Short Gun 25

Close up of shotgun fired and shell ejected from chamber

JESHI la Polisi mkoani Simiyu limekamata silaha aina ya Short Gun zipatazo 25 zilizotengenezwa kienyeji  na  risasi tano za Short Gun.

Silaha hizo zimekamatwa baada  ya operesheni  na misako iliyofanyika mkoani humo yenye lengo la kuzuia uhalifu.

Kamanda wa Polisi mkoani Simiyu, Blasius Chatanda akizungumza leo Novemba 23, 2022 amesema katika kipindi cha mwezi Januari hadi Oktoba mwaka huu jeshi hilo limefanya  operesheni mbali mbali na kukamata silaha zilizokuwa zinamilikiwa kinyume na sheria  zikiwemo ‘riffle’  tatu.

Advertisement

Aidha,  Chatanda ametoa wito kwa wananchi wa Mkoa huo,  kuendelea kutoa taarifa endapo wataona viashiria vya uhalifu, waharifu na kwamba wafike pia Mahakamani pindi wanapohitajika kutoa ushahidi ili kuisaidia mahakama kufikia maamuzi ya kutenda haki.