JESHI la Polisi Mkoa wa Arusha, limefanya ukaguzi wa magari ya shule mbalimbali mkoani humo, ambapo zaidi ya magari 150 yamekaguliwa, huku wamiliki na madereva wa magari hayo wakipewa elimu.
Akiongoza shughuli hiyo, leo Jumatatu Septemba , 2022, Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha, Mrakibu wa Polisi, Solomon Mwangamilo, amesema kazi hiyo itakuwa endelevu na kuonya wamiliki ambao magari yao hayatakaguliwa.
Amesema ukaguzi huo na elimu kwa wamiliki na madereva utasaidia kupunguza ajali, ambazo zimekatisha ndoto za vijana ambao ni hazina kwa Taifa.