Polisi yashikilia wawili mauaji ya mtoto Bukoba

POLISI mkoani Kagera inawashikilia watu wawili wakazi wa Bukoba kwa tuhuma za mauaji ya mtoto wa miaka mitatu mkazi wa Mtaa Matopeni, Kata ya Kashai mkoani humo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera,  William Mwampaghale alisema watuhumiwa hao ambao hakuwataja majina sababu za kiusalama, wanatuhumiwa kumuua mtoto Aisha Issa kwa kutumia kamba Septemba 29, mwaka huu.

Alisema baada ya tukio hilo mtuhumiwa mmoja alitoroka, lakini huyo mwingine alikamatwa na kumtaja mwenzake, ambaye alikamatwa juzi jioni.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x