Polisi yatangaza nafasi mpya za ajira

MKUU wa jeshi la polisi nchini, IJP camillus wambura ametangaza nafasi mpya za ajira kwa vijana wataokidhi vigezo vilivyotajwa kupitia barua iliyotolewa na ofisi yake.

Katika taarifa yake iliyotolewa Julai 18, 2023 IJP Wambura ametaja vigezo mbalimbali huku kigezo (a) mwombaji anatakiwa kuwa raia wa Tanzania (b) awe amehitimu kidato cha nne kuanzia mwaka 2019-2022 kwenye umri kuanzia miaka 18-25.

IJP Wambura ameeleza mwombaji anatakiwa awe amemaliza kidato cha nne na kupata ufaulu wa daraja I-IV na kwa mwombaji mwenye daraja la IV anapaswa kuwa na ufaulu wa pointi 26-29.

Habari Zifananazo

4 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button