Pombe haramu yaua 34 India

NEW DELHI: WATU 34 wamekufa na wengine zaidi ya 100 kupelekwa hospitali baada ya kunywa apombe haramu katika Jimbo ya Tamil Nadu Kusini mwa India.

Shirika la Habari la Press Trust la India limesema watu hao wamekunywa pombe yenye kiambato cha kikemia.

Habari zimesema zaidi ya watu 100 waliopata matatizo ya kutapika, maumivu ya tumbo na kuhara walilazwa katika hospitali ya wilaya ya Kallakurichi na zaidi ya 60 bado wanapatiwa matibabu.

Mkuu wa polisi ni miongoni mwa maafisa 10 waliachishwa kazi katika wilaya hiyo kuhusiana na tukio hilo.

Mwaka uliopita, zaidi ya watu 10 walikufa katika tukio kama hilo katika wilaya jirani katika Jimbo la Tamil Nadu.

Habari Zifananazo

Back to top button