DAR ES SALAAM: NYOTA wa maigizo na mitindo, Jacqueline Wolper amesema ameamua kuachana na unywaji wa pombe rasmi kwa kuwa haina faida kwake zaidi ya hasara.
Wolper amesema kuwa anapokunywa pombe hujikuta anaongea maneno yasiyofaa, ha ha ha…, hapa ngoja kwanza n’cheke, maana nimekumbuka maneno ya wahenga “pombe sio chai”
Katika tukio linalofanana na hili, mwezi Mei, 2023 Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu pia alitangaza kuachana na matumizi ya pombe.