Ponyo ajiondoa urais, aungana na Katumbi
WAZIRI Mkuu wa zamani wa DR Congo, Augustin Matata Ponyo, amejiondoa kwenye uchaguzi wa urais utakaofanyika mwezi ujao.
Ponyo amesema baada ya hatua hiyo sasa atamuunga mkono Moïse Katumbi, mfanyabiashara milionea na gavana wa zamani wa eneo la Katanga.
Wawakilishi wa vyama vikuu vya upinzani nchini nchini humo walifanya mazungumzo mapema wiki hii kuhusu jinsi ya kuhakikisha uchaguzi huo utakuwa wa haki, na kuchunguza uwezekano wa kuwepo kwa mgombea mwenza kumpa changamoto Rais Felix Tshisekedi.
Ponyo amesema anaamini wagombea wengine wa upinzani watafuata nyayo zake kujiondoa kumuunga mkono Katumbi.