Potter athibitisha “Pulisic nje kwa miezi kadhaa”

KOCHA wa Chelsea, Graham Potter amethibitisha kuwa kiungo wa pembeni, Cristian Pulisic ameumia na atakuwa nje ya uwanja wa miezi kadhaa.

Potter amesema mshambuliaji Raheem Sterling naye atakuwa nje ya uwanja kutokana na majeraha, lakini matumaini yake hakitokuwa kipindi kirefu, ameongeza kuwa wanasubiri ripoti ya madaktari kuthibitisha ukubwa wa tatizo lake.

Kocha huyo raia wa Uingereza amesifu uwezo wa Joao Felix aliyesajiliwa leo kwa mkopo akitokea Atletico Madrid, kwa kusema kuwa ni mchezaji ambaye anaweza kuleta mabadiliko ndani ya klabu hiyo.

Chelsea kwa sasa inakabiliana na kundi kubwa la wachezaji majeruhi, akiwemo Ng’olo Kante, Reece James, Eduardo Mendy, Mason Mount, Wesley Fofana, Ben Chilwell na Armando Broja.

Habari Zifananazo

Back to top button