Potter atishiwa maisha

Kocha wa Chelsea, Graham Potter amefichua kuwa alipokea vitisho vya kuuawa, lakini amesisitiza haikumuathiri kisaikolojia kwani analenga kubadilisha mwenendo wa klabu.

Potter alisema kuwa alishambuliwa kwa njia ya barua pepe, akisema: “Kama vile nimekuwa nikiungwa mkono nimekuwa na barua pepe zisizo nzuri sana ambazo zilinitaka kufa na kutaka watoto wangu wafe, kwa hivyo ni wazi kwamba hiyo haipendezi.”

Potter yuko kwenye presha kubwa Stamford Bridge kufuatia kichapo cha 1-0 Jumamosi iliyopita dhidi ya Southampton inayoshika mkia kwenye Ligi Kuu ya England.

Timu yake, ambayo inashika nafasi ya 10 kwenye ligi, imeshinda mara mbili pekee katika michezo 14 iliyopita na imefunga bao moja nyumbani mnamo 2023.

“Changamoto kwangu ni, ‘Sawa, ninajiendeshaje?’ Hiyo ndio huwa naigeukia. Kadiri unavyozidi kwenda juu ndivyo unavyozidi kuwa na presha ya jinsi ulivyo mtu. Nataka kufanikiwa hapa.” Amesema Potter.

Habari Zifananazo

Back to top button