PPFT yamuunga mkono Rais Samia

MWENYEKITI wa Ushirika wa Wachungaji wa Kipentekoste Tanzania (PPFT) Askofu Pius Ikongo ametangaza kumuunga mkono Rais Samia Hassan Suluhu kwa kauli yake ya kutamka na kufunga mjadala wa bandari

Akizungumza na waandishi wa habari jana Jijini Arusha, Askofu Ikongo amesema kila mmoja ametoa maoni kuhusu suala la bandari na endapo kuna kasoro katika mkataba huo zirekebishwe kwa maslahi ya nchi.

Amempongeza Rais Samia kwa kutoa kauli ya kunyamaza kimya lakini aliongezakwa kusema kuwa kunyamaza kimya huko kunatoa nafasi ya watu wengine kuendelea kujadili ilhali suala hilo limejadiliwa sana basi ifike ukomo wake

Advertisement

“Rais anaponyamaza utulivu unakuwepo na kila mtu ameongea lakini kwasababu Rais ametoa nafasi sipingani nao lakini sasa Rais atamke kwakusema sasa basi amepokea maoni ya kila aliyesema kuhusu bandari sasa iwe mwisho”

4 comments

Comments are closed.

/* */