PPRA waendesha semina usimamizi fedha za serikali

MAMLAKA ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) kwa kushirikiana na mashirika yasiyo ya kiserikali ya Omuk Hub na Africa Freedom of  Information Center (AFIC) wameedesha semina kwa viongozi  wa idara mbalimbali ,vyama vya siasa katika Wilaya ya Bukoba kwa lengo la kusimamia fedha asilimia 30 inayotolewa na Serikali ili kunufaisha makundi maalum.

Viongozi Mbalimbali wa Wilaya Bukoba  wakiwemo madiwani Manispaa ya Bukoba, viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) pamoja na viongozi wanawake, wataaalam ofisi ya mkuu wa wilaya  wamepatiwa semina  ya mafunzo ya manunuzi ya umma  asilimia 30 ya fedha za umma ambazo zinatoka Serikali Kuu  kwa ajili ya kuwezesha vikundi vya  wanawake ,vijana ,wazee na watu wenye ulemavu  ili kupata tenda za miradi  mbalimbali  katika jamii.

Akizungumza wakati wa kufungua semina ya mafunzo ya siku mbili ndani ya Manispaa ya Bukoba   Winfrida Samba ambaye amemwakilisha Mkurugenzi wa PPRA alisema mafunzo hayo kwa Mkoa Kagera  yanalenga kutoa mwanga wa kuunda vikundi vya vikundi maalum na kuondoa changamoto ya ajira kwa watu wasio na ajira.

Advertisement

“Tukiongelea katika nchi hii kila bajeti inayotengwa halmashauri asilimia 30 ya miradi yote ya umma utengwa fedha ya kutoa tenda kwa vikundi vilivyosajiliwa kisheria kwa makundi haya niliyotaja hivyo naomba tuchangamkie fursa hii kwa sababu katika tenda hizo za kazi mbalimbali wanawake wanapata asilimia 10 ya miradi kwa ajili ya kutekele, vijana asilimia 10, wazee asilimia 5 na watu wenye ulemavu asilimia 5 tujisajili ili tunufaike na  fedha za serikali”. alisema Samba

Mkurugenzi wa Omuka Hub  Mbunge wa Viti Maalumu kutoka Mkoa wa kupitia Asasi za Kiraia NGO’s Tanzania Bara, Neema Lugangira alisema kuwa Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu inawawezesha kuwapatia watu uelewa juu ya manunuzi ya umma aslimia 30 na zoezi hilo litashuka katika wilaya nyingine za mkoa huo pamoja na maeneo mengine na kusema kuwa Watanzania wandelee kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan kwa furusa nyingi anazo enda nje ya nchi kwani zina zaa matunda na kufungua nchi.

Alisema matamanio yake kuona wanawake wengi na vijana wananufaika na asilimia 30 inayotengwa kwani asilimia kubwa ya wanawake ukimbilia halmashauri kutafuta mkopo wa asilimia 10 ambao hauna riba wakati fedha nyingine za serikali zipo pale  kusaidia maelfu ya wanawake wengi endapo watajitokeza kujisajili na kuunda vikundi vinavyotambulika kisheria.

Mkurugenzi wa mtendaji kutoka Africa Freedom of Information Center (AFIC) Gilbert Sendugwa kutoka nchini Uganda alisema utafiti uliofanywa na shirika hilo katika maswala ya manunuzi umma kwa kuomba tenda serikalini kwa nchi tano za Africa Ethiopia, Tanzania, Uganda , Rwanda na Kenya wamebaini kuwa  vikundi vya wanawake vinavyoomba tenda za miradi fedha inayotengwa na serikali kwa ajili ya makundi maalumu ni asimilia moja ya wanawake wanaojitokeza kuomba kazi hizo .

Aidha utafiti unaonyesha kuwa uwezo wa wanawake kumiliki biashara zao kwa nchi za Ethiopia ni asilimia 36.2,Uganda asilimia  38.2,Rwanda asilimia 37, Kenya asilimia 48 na Tanzania ikiongoza kwa asilimia 48.1 ambapo aliwaomba viongozi waliopatiwa mafunzo kuendelea kuzisimamia halmashauri na kutoa kazi hizo kwa vikundi vilivyotimiza  masharti kuomba Kazi hizo ili kuongeza vipato katika jamii