Prof. Janabi awakumbuka wafanyakazi Christimas
DAR ES SALAAM: MKURUGENZI Mtendaji Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Mohamed Janabi, ametoa zawadi kwa wafanyakazi wake kwaajili ya Kusherehekea Sikukuu ya Christmas na Mwaka Mpya.
Christmas itakuwa Jumatatu ya wiki ijayo ambapo wakristo wote ulimwenguni watasherehekea sikukuu hiyo ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo.
Janabi ametoa zawadi hiyo kwa wafanyakazi wake 3,500 wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Upanga na Mloganzila.
Zawadi zilizotolewa ni sukari kilo tatu, mafuta ya kupikia lita moja na miche miwili ya sabuni kwa kila mmoja.