Prof Janabi: ‘Tunzeni Figo’

sukari, wanga adui namba moja

DAR ES SALAAM: WIMBI la wagonjwa wa kusafisha figo limezidi kuongezeka na kwamba kwa siku hospitali ya Taifa ya Muhimbili inahudumia wagonjwa 120 hadi 130 hivyo jamii kutakiwa kuchukua tahadhari na kufuata mtindo bora wa maisha.

Akizungumza, Mkurugenzi wa Muhimbili, Prof Mohamed Janabi amesema vitu hatari zaidi kwenye mwili ni sukari na wanga na wala si mafuta kwa sababu mwili hautunzi wanga wala sukari bali huvibadilisha kuwa mafuta.

Ametaka watu kupunguza matumizi ya vitu vyenye sukari, na sukari yenyewe.

“Sukari ni ugonjwa hausababishwi na fangasi, hausababishwi na bacteria, unasababishwa na lishe, lazima tubadilishe mtindo wa maisha, mtakaopata nafasi mzungumze na mtu anayefanyiwa dialysis (kusafisha figo) ndio mtafahamu umuhimu wa kutunza figo,”amesema Janabi na kuongeza

“Ni kitu ambacho unaweza kukiepuka, kula mlo mmoja unabana matumizi milo miwili, huitajji kwenda gym unahitaji kutembea hatua 10,000 kwa siku, punguza vitu vya sukari bei ya sukari imepanda juu ‘take advantage’.”amesema Janabi

Aidha, amesema MNH kwa siku inasafisha wagonjwa wa figo 120, -130 na kwamba ‘session’ (kipindi ) ya kwanza inaanza saa 11 kamili asubuhi wagonjwa wanaanza kufika kuanzia saa tisa usiku na inakwenda kwa saa nne.

“Wanatoka hao wanaingia ‘session’ ya pili baada ya kuweka dawa kwenye mashine, inaisha saa tisa hadi saa 10 na session ya mwisho inamalizika za mbili usiku kila siku.

“Ukitoka yale masaa manne uchovu wake kama mtu aliyekimbia marathon.

Kwa wagonjwa 130 asilimia 90 ni kwa sababu ya shinikizo la juu la damu ikifuatiwa na kisukari,”amesisitiza Prof Janabi

Habari Zifananazo

Back to top button