Prof. Jay akaribia kufyatua mambo
MSANII wa hip hop nchini Joseph Haure ‘Prof Jay’ ameweka bayana ujio wake mpya hivi karibuni baada ya kuwa nje ya tasnia hiyo kwa muda mrefu kutokana na kuugua.
Ametoa kauli hiyo baada ya kutembelewa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Dk Kedmon Mapana nyumbani kwake Mbweni, Dar es Salaam na kusema wamezungumza mengi sana kuhusu sanaa ya Tanzania hasa suala la kufungia ya nyimbo za wasanii.
Prof Jay amemwambia Katibu Mtendaji wa Basata kuwa ni walezi na sio polisi na kutoa ahadi kuwa atamsikia tena hewani siku si nyingi na watu wake tayari.
“Nilitembelewa na Katibu mtendaji Dk Kedmon Mapana nyumbani kwangu Mbweni, tuliyajenga mengi sana kuhusu sanaa yetu hasa fungia nyimbo za wasanii maana Baraza la sanaa ni walezi na sio polisi, pia nilimuahidi atanisikia tena hewani siku si nyingi,”amesema Prof Jay