Prof. Kahyarara atembelea Banda la TCAA

ZANZIBAR: Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi Prof. Godius Kahyarara ametembelea Banda la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) ambapo amepata maelezo kuhusu Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) katika maonesho ambayo ni sehemu ya maadhimisho ya Miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yanayofanyika katika viwanja vya Fumba, Zanzibar.

Prof. Kahyarara aliambatana na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Dk. Ali Possi alipokelewa na Mkurugenzi wa Huduma za Mamlaka TCAA ,Teophory Mbilinyi ambapo alimpatia maelezo juu ya mradi huo pamoja na kozi mbalimbali zinazotolewa na chuo hicho.

Kwa upande wake ,Prof Kahyarara ameipongeza TCAA kwa usimamizi mzuri wa Sekta ya Usafiri wa Anga na kuahidi serikali itaendelea kuwekeza katika sekta hii muhimu pia alisisitiza chuo kuendelea kujitangaza zaidi ili kisikike na kuwafikia watu wengi zaidi ndani na nje ya nchi.

@catc_tanzania ni moja ya vyuo vinavyotoa kozi ya Usalama wa Usafiri wa Anga (ASTC) na ni moja kati ya vyuo tisa vyenye sifa hizo Afrika na 35 duniani.

 

Habari Zifananazo

Back to top button