Prof. Mkenda: Mfumo mpya elimu utasaidia kujiajiri

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf  Mkenda,  amesema kuanzia mwakani elimu ya msingi itakuwa miaka sita na sekondari miaka minne, ili kuwapa fursa wanafunzi kuchagua aina ya masomo yanayopenda, kusaidia waweze kujiajiri wamalizapo masomo.

Mkenda ameyasema hayo jijini Arusha, wakati akifungua maonyesho ya Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi(NACTVET), yanayoshirikisha taasisi zaidi ya 200 zikiwemo za serikali na binafsi.

Amesema mabadiliko hayo yataenda sambamba na kufundisha lugha ya kingereza, ambayo iitaanza kufundishwa kuanzia darasa la kwanza na baada ya darasa la sita kutakuwa na mkondo wa mafunzo ya elimu na ufundi stadi utakaojulikana kama elimu ya amali na elimu ya jumla.

Kila mkondo kutakuwa na michepuo yake, ili kuwapa nafasi wanafunzi kuchagua masomo wanayoyataka kwa ajili ya kuendeleza ujuzi na nadharia zaidi ili wakimaliza shule waweze kujiajiri wenyewe.

“Kuanzia mwakani watoto watasoma hadi darasa la sita na watafundishwa lugha ya Kingereza na Kiswahili na masomo mengineyo, lakini pia kutokana na mitaala kubadilika watoto wataweza kuonesha umahiri wao katika masomo yao, ” amesema.

Naye Katibu Mtendaji NACTVET, Dk Adolf Rutayuga, alisema vyuo vya ufundi vinaandaa mitaala na kuihuisha mara kwa mara kutokana na mahitaji ya soko la ajira.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x