Prof Muhongo: Mchango wa sekta ya madini bado mdogo

Ataka watanzania wasifurahie asilimia 16 ya hisa

MBUNGE wa Musoma Vijijini, Prof. Sospeter Muhongo amewataka wabunge kuacha kushangilia mabilioni ya sekta ya madini kwani fedha hizo ni ndogo tofauti na wanavyozisikia.

Amesema, wanaelezwa mabilioni ya fedha kama mtu hana uzoefu ataona ni fedha nyingi lakini ni wazi sekta ya madini haijachangia ipasavyo.

Akichangia mjadala wa bajeti ya Wizara ya madini leo Aprili 28, 2023, Prof Muhongo amesema sekta ya madini ingechangia ipasavyo ukuaji wa uchumi unaopaswa kuondoa umaskini lazima ukue kwa asilimia nane mpaka 10 ukiwa chini ya hapo hata ukifurahije hautotoka kwenye umaskini.

“Umaskini wetu lazima upungue kutoka asilimia 20 mpaka 10 na, na watakaotupeleka huko ni sekta ya madini, gesi na mafuta.”Amesema Muhongo na kuongeza

“Sasa tangu mwaka 1961 mpaka mwaka 2021 ni miaka 60 sekta ya madini muda mwingi imejishughulisha na  masuala ya usimamizi wa madini ‘administration of mining sector’ ndio maana madini yanayochimbwa ndio hayo hayo miaka nenda rudi yaani dhahabu, almasi, na vito Tanzanite na rubi, ndio maana Liganga na mchuchuma nitaongea siku nyingine.

“Wasingeshughulika na utawala sana, chuma na liganga toka miaka ya 60 tungeshachimba, uchumi wa dunia wa leo wa dunia ni wa aina mbili ni ‘private and worth capitalism’ ya ubinafsi, uchumi mwingine ulioibuka sana ni ‘state capitalism’

“Inafanywa China na imefanikiwa, India, Brazil, Norwary inafanikiwa….Norwary kampuni tunayofanya nayo gesi hapa nchini ni ya serikali iyo ndio inaitwa state capitalism.”Amesema Muhongo  na kuongeza

“Sekta ya madini ni lazima itupeleke huko, ni lazima uwepo mgodi unaomilikiwa kwa asilimia 100 na serikali la sivyo hatutatoka na mtadhani hizo bilioni ni hela nyingi sana wakati hamna kitu.”Amesisitiza

Aidha, amesema ni wakati sasa wa serikali kuanzia sasa ijihusishe na uwekezaji, katika taasisi mbili muhimu ambayo ni ya kwanza ni ‘geological survey’.

“Ni ajabu Tume ya Madini inapewa umuhimu bado ni makosa yale yale ya kujihusisha na utawala wa madini badala ya kujiwekeza kwenye ‘geological survey’ ni lazima tuwekeze ndio itatuambia tuna madini ya aina gani, kiasi gani.

“Lakini ‘geological survey’ haijawekezwa, vile vile wizara ya madini sio lazima ione hii ni wizara ya elimu, ukitaka wataalamu nenda Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, nenda Mzumbe wataalamu mtawakuta huko lakini hawana vifaa, kawekezeni kwenye maabara vyuoni huko.”Amesema

Amesema Tanzania hatuna maabara inayoweza kusaidia katika eneo hilo na badala yake wasipowekeza wataendelea kupokea ripoti kutoka nje ambazo hawawezi kuzipitia.

Aidha, eneo la pili ambalo Profesa Muhongo ametaka lifanyiwe marekebisho ni sheria kwa kuwa nyingi zina mapungufu.

“Sheria zetu nyingi zina mapungufu  ila kuna hii moja ya asilimia 16 ya hisa, waheshimiwa wabunge na watanzania kwenye hiyo asilimia 16 mnayoshangilia tunaweza tusipate kitu.

“Hatuko kwenye bodi inayofanya maamuzi, menejimenti ya juu haupo, haujui unazalisha kiasi gani, haujui unauza kiasi gani, wewe umekaa pembeni unasubiri uletewe fedha eti una hisa asilimia 16 maana ya kuwa mwanahisa ni kwamba ni lazima ushirikiane na mwenzao kuwekeza, kwenye faida mshirikiane na kwenye hasara.”Amesema Prof. Muhongo

Amesema ili Wizara ijifunze, inapaswa kwenda Mgodi wa Mwadui na kuchukua ripoti ya mtaalamu marehemu Alnoor Kassam Mtanzania aliyesoma Uingereza na alikuwa anafanya kazi nchi za nje lakini Hayati Julius Nyerere  akamrudisha nchini  mwaka1969 na kumpeleka Mwadui akachunguze kwa kuwa alikua anataka kuitaifisha.

“Mwalimu alimwambia tunataka kutaifisha, ebu tuambie, kwa kifupi alitoa ripoti Watanzania hawaelewi nini kinaendelea Mwadui, Mwadui tulianza na share (hisa) 50 kwa 50 wakasema wanajenga ‘Plant’ mpya ya kisasa, Tanzania wakambiwa toa hela hawana, ‘share’ zikashuka kutoka 50 hadi 25, kwa hiyo Mwadui mpaka leo sijui kama Tanzania tuna ‘share’ hata moja kama serikali.

“Sasa hili la hisa asilimia 16 lazima tulirekebishe uwenda tusipate kitu au tukapata kidogo

Aidha, eneo la tatu ambalo Profesa Muhongo ameonyesha wasiwasi ni umakini huku akihoji leseni zinazotolewa za ‘platinum group metals’ na kueleza kuwa  ‘group’ hilo lina  ina ya madini kama saba ikiwemo ‘Platinum’, na kuhoji “tunapowapa kibali tunajua wanaenda kutoa nini?

“Kwenye hii group hili pia kuna madini yanaitwa Rodium, wakati dhahabu ilikuwa dola 1,850 rodium ilikuwa dola 10,300 je sisi tunajua tuliowapa leseni watayachimba hayo?

“Unakuja kwenye ‘rare Earth Element’ madini ya mkakati, je ni ya mkakati kwako au kwa wawekezaji? Amehoji na kuongeza

“Ndani yake humo kuna madini 17 kama hufahamu utakuwa unaongea ongea tu, na yote yana thamani kubwa….; “Ingekuwa ni mimi  badala ya kuwekeza kwenye utawala wa madini  ningewekeza kwenye ‘geological survey’

Aidha, Prof. Muhongo amesema kuwa ameenda kwa wale wanaotukopesha Benki ya Dunia kuangalia hisa zao ambazo zinaendana na ‘voting power’ jinsi unavyokuwa na hisa nyingi kura yako ndio inavyokuwa na nguvu.

“Sasa benki ya dunia Marekani ‘voting ni around 17percent’, Japan ni around 8.5 5 percent, China ni 2.25 percent sasa angalia Marekani yenye voting power kubwa ana hakiba ya dhahabu tani 8,133 uyu Japani ana tani 846 China ana akiba ya tani ya dhahabu 1,948 wewe Tanzania kwa nini bado una sita, Wizara ya Madini na Benki Kuu kwa nini bado mnasita? alihoji

“Nimalizie lazima tuwe na hiyo ‘refinery’ mbili Geita ina ‘process’ kilogramu 600 kwa siku Mwanza 400 kwa siku lakini waheshimiwa wabunge hii ‘refineries’ hazina madini na uwenda zikafungwa.”alisema Muhongo na kushangiliwa kwa nguvu na wabunge.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x