Prof Shaba, aliyemfanyia uchunguzi Sokoine afariki

MAREKANI: DAKTARI Bingwa wa utambuzi wa magonjwa na sababu za vifo, Profesa James Shaba amefariki dunia jana jumanne Desemba 5, 2023.
Profesa Shaba ndie aliyefanya uchunguzi wa mwili wa Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania ‘postmortem’ Hayati Edward Sokoine, kwenye hospitali ya Muhimbili.

Sokoine alifariki Aprili 12, 1984 akiwa na umri wa miaka 45 kutokana na ajali ya gari iliyotokea Dakawa mkoani Morogoro.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na familia ya Profesa Shaba inasema kuwa alifariki majira ya saa mbili usiku, Chicago nchini Marekani alipokuwa akiishi.

Mtoto wa marehemu, Anale Shaba amesema taratibu za maandalizi ya mazishi zitatolewa baadaye na kwamba marehemu Shaba ameugua kwa muda mrefu.

Habari Zifananazo

Back to top button