Prof. Silayo amteua Malyango kuwa Naibu Kamishna TFS

KAMISHNA wa Uhifadhi wa Wakala wa Misitu (TFS) Profesa Dos Santos Silayo amemteua na kumpandisha cheo Dk Abel Malyango Masota kuwa Naibu Kamishna na Mkurugenzi wa Usimamizi wa Rasilimali za Misitu.

Kabla ya uteuzi huo SACC Dk Abel alikuwa akikaimu nafasi hiyo. Taarifa iliyotolewa na kitengo cha mawasiliano cha TFS leo, imeeleza kuwa uteuzi huo ulianza Machi 1, 2023.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa Prof Silayo amemteua na kumpandisha SACC Caroline Gracewell Malundo kuwa Naibu Kamishna na Mkurugenzi wa Uzalishaji mbegu za miti.

Kabla ya uteuzi huo Caroline alikuwa Kamanda wa TFS Kanda ya Mashiriki.

Habari Zifananazo

Back to top button