Profesa James Mdoe akikata utepe kuzindua Maktaba ya Mkoa wa Iringa

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa James Mdoe akikata utepe kuzindua Maktaba ya Mkoa wa Iringa jana, baada ya kufanyiwa ukarabati. Serikali imetumia zaidi ya shilingi bilioni moja kukarabati maktaba katika mikoa saba nchini. Wa pili kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Huduma za Maktaba nchini, Dk Mboni Ruzegela. (Na Mpigapicha Wetu).