Profesa Mahalu amsifu Samia diplomasia ya uchumi

BALOZI na mwanasheria nguli, Profesa Costa Mahalu ameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutekeleza kwa vitendo diplomasia ya uchumi.
Profesa Mahalu amesema mikakati ya serikali itawafanya mabalozi wa Tanzania katika nchi mbalimbali kuacha kuhudhuria hafla tu na badala yake sasa watakuwa na shughuli ya kutangaza bidhaa za Tanzania na kutafuta masoko.
Alisema hayo nyumbani kwake Dar es Salaam katika mahojiano na waandishi wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN), Daily News na HabariLEO.
Profesa Mahalu alisema Rais Samia anafanya vizuri katika diplomasia ya uchumi na ameonesha anavyotaka wanadiplomasia waende na wakati.
“Nimekuwa mwanadiplomasia miaka 20 sasa na kwa kweli nimevutiwa na mtazamo wa Rais Samia katika hili, ni mzuri anataka twende na wakati,” alisema.
Aliongeza: “Unapokwenda nje ya nchi kama balozi wewe ni mwakilishi binafsi wa Rais, unapokwenda kule serikali ya kule inakupokea na kukupa hadhi nzuri tu lakini pia kazi yako nyingine ni kusaidia Watanzania walioko katika nchi hiyo.”
Profesa Mahalu alisema nchi nyingi duniani zilishaanza kutekeleza diplomasia ya uchumi hivyo amepongeza jitihada za Rais Samia kwa kuitekeleza kwa vitendo.
Alisema ili diplomasia hiyo itekelezeke kama Rais anavyotaka ni lazima kuwe na utayari wa kuanzia wizara na wafanyabiashara ili kuhakikisha Tanzania inazalisha bidhaa bora zinazokubalika kimataifa.
“Niseme tu ukweli, sasa hivi kuna ushindani mkubwa baina ya nchi na nchi kama Kenya, Afrika Kusini, Nigeria, Botswana, Namibia na nyinginezo ambao wakiuza bidhaa zao zinakuwa za viwango vya juu, sasa tuwe na huu utayari wa kukabili ushindani,” alisema Profesa Mahalu.
Alisema alipokuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia alijitahidi kwa kiasi fulani kukutanisha wafanyabiashara wa Tanzania na wenzao wa Ugiriki, Uturuki, Slovakia na Italia.
“Tulijitahidi ili kuweka misingi mizuri kwa wenzetu watakaokuja baadaye kwa kuwa watakuwa wanafahamu vyema diplomasia ya uchumi ni kuhakikisha kwamba nchi unayoiwakilisha katika masuala ya uchumi waelewe ulipo kuna fursa gani na kupitia wewe balozi waelewe soko la bidhaa fulani likoje,” alisema Profesa Mahalu.
Alisema pia alijaribu kuangalia masuala ambayo Tanzania inaweza kujifunza katika eneo la viwanda hasa kwa kuwa Tanzania ni tajiri wa rasilimali nyingi.
“Balozi unasukumwa watu kuwa wana ari ya kupata fursa ya kuuza, na wewe unatafuta soko kama vile korosho, asali, samaki zilikuwa bidhaa zinazotafutwa sana. Sasa huku nyumbani unasema unahitaji kontena mbili za korosho au asali lakini baada ya mwezi bidhaa hazionekani kweli hili limetuaibisha sana,” alisema Profesa Mahalu.
Alisema Ugiriki na Italia kuna kipindi walikuwa wakihitaji korosho na kwa kuwa walikuwa wanamuamini yeye walikuwa wanaagiza na walipokosa walilaumu.
Profesa Mahalu alisema diplomasia ya uchumi ni muhimu katika ujenzi wa uchumi wa nchi lakini inahitaji utayari wa nchi na wananchi kufanikisha hilo.
Hivi karibuni Rais Samia alipokuwa akiwaapisha viongozi wakiwemo mabalozi John Ulanga na Said Yakubu alionesha utayari wake kuitekeleza diplomasia ya uchumi kwa kuanzisha idara ya diplomasia ya uchumi katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
UBUNIFU – ALILIA NA KUPAMBANA KUANDIKWA/KUYAUWA MAGAZETI YA GROBAL PUBLISHER
UBUNIFU – ALILIA NA KUPAMBANA KUANDIKWA/KUYAUWA MAGAZETI YA GROBAL PUBLISHER…
UBUNIFU – ALILIA NA KUPAMBANA KUANDIKWA/KUYAUWA MAGAZETI YA GROBAL PUBLISHER….
UBUNIFU – ALILIA NA KUPAMBANA KUANDIKWA/KUYAUWA MAGAZETI YA GROBAL PUBLISHER… ….
UBUNIFU – ALILIA NA KUPAMBANA KUANDIKWA/KUYAUWA MAGAZETI YA GROBAL PUBLISHER.. … .
UBUNIFU – ALILIA NA KUPAMBANA KUANDIKWA/KUYAUWA MAGAZETI YA GROBAL PUBLISHER… …… …
UBUNIFU – ALILIA NA KUPAMBANA KUANDIKWA/KUYAUWA MAGAZETI YA GROBAL PUBLISHER……………….
UBUNIFU – ALILIA NA KUPAMBANA KUANDIKWA/KUYAUWA MAGAZETI YA GROBAL PUBLISHER…………………………..