Profesa Mbarawa aitaka TPA kutangaza maboresho bandari ya Mtwara

WAZIRI wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa amewataka Mamlaka ya Bandari Nchini (TPA) kutangaza maboresho makubwa ambayo yamefanyika katika bandari ya Mtwara ili iweze kutumika ipasavyo.

Amesema hatua hiyo itasaidia kuhakikisha Bandari ya Mtwara inaendelezwa na kuwa kituo kikubwa cha usafirishaji katika ukanda wa kusini na nchi za jirani.

Makame ametoa wito huo leo wakati alipotemebelea bandari ya Mtwara kuangalia utendaji katika bandari hiyo.

“Watu wa TPA haya mambo mazuri nendeni mkayatangaze , mkawaambie wafanyabiashara kwamba bandari ya Mtwara sasa imefunguka ,gharama za usafirishaji zimepungua Kwa asilimia kubwa,” amesema.

Mbarawa amesema TPA wakitangaza bandari ya Mtwara ndani ya nje ya Tanzania wafanyabiashara wengi watakuja na kuhakikisha bandari hiyo inafanya kazi usiku na mchana.

Baadhi ya gharama zilizopunguzwa ni za gharama za kusafirisha mizigo kwenye meli (wharfage charges) kwa nusu gharama ikilinganishwa na baadhi ya bandari hapa nchini, gharama za kupakia na kupakua mizigo kutoka kwenye meli kwenda kwenye gati Kwa asilimia 70.

Pia katika bandari ya Mtwara, serikali imeongeza siku za mzigo kukaa bandarini.

Serikali pia imeweka vifaa vyote muhimu vya kuwezesha usafirishaji ikiwemo kifaa Maalumu cha kupakua na kupakulia makontana (Ship to Shore Container Crane).

Habari Zifananazo

Back to top button