Profesa Mbarawa mgeni rasmi Siku ya Wahandisi

MSAJILI wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB), Benard Kavishe amesema wahandisi 4,300 wanatarajia kushiriki Siku ya Wahandisi Tanzania 2022 itakayoadhimishwa kwa siku mbili jijini hapa kuanzia leo.

Akizungumza na waandishi wa habari Jumatano, Kavishe alisema wahandisi 3,500 wanatakiwa kushiriki moja kwa moja na wengine 800 wamejisajili kwa ajili ya kushiriki kupitia mtandao.

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa ndiye anayetarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo.

Alisema Jumuiya ya Wahandisi Tanzania inaadhimisha Siku ya Wahandisi kwa mara ya 19 tangu kuzinduliwa mwaka 2003, lengo likiwa ni kuiwezesha jumuiya hiyo kuonesha umma nini wahandisi wa Tanzania wanaweza kufanya katika kuleta maendeleo ya nchi.

Kavishe alisema katika maadhimisho hayo wahandisi 400 watakula kiapo cha wahandisi wataalamu na kuwapa zawadi  wahandisi 36 waliofanya vizuri katika mitihani yao ya mwaka wa mwisho kwa mwaka 2021/23.

 

 

 

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x