Serikali yafafanua kutotangazwa kwa shule bora

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda ameunga mkono uamuzi wa Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA) wa kutotangaza shule na wanafunzi bora kwamba utaratibu huo ulikuwa ukikosolewa na wataalam wa elimu.

Profesa Mkenda amesema hayo leo Februari Mosi, 2023 bungeni jijini Dodoma baada ya kuombwa mwongozo na Mbunge wa Bunda Vijijini (CCM), Mwita Getere.

Getere amesema kumekuwa na minong’ono kuwa kutotangazwa kwa mpangilio wa ufaulu kutadhoofisha elimu ya Tanzania.

Advertisement

“Kwa kuwa Serikali imo humu ndani kwanini isitoe taarifa humu ndani kipi bora.

Hayo matangazo waliositisha yanaumuhimu gani kwa wananchi na yana ubora gani kwa wananchi,” ameuliza.

Akipokea na kuibu mwongozo huo, Profesa Mkenda amesema baraza hilo limeacha kupanga shule kwa ubora kutoka na sababu ya utata wa jambo hilo.

“Chukua shule ambayo inawatoto 100, nyingine ina wanafunzi 20, wamemaliza kidato cha nne, wanafunzi 170 wapata alama A, 30 hawakupata A, wenye wanafunzi 20 wote wamepata A kwa kuangalia wastani ufaulu ni wazi wenye wanafunzi 20 itatangazwa ni shule bora.” amesema Mkenda.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *