Profesa Mkumbo: Bandari haijauzwa

MBUNGE wa Ubungo Profesa Kitila Mkumbo (CCM) amesema Azimio lililowasilishwa na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi halihusu kuuzwa kwa bandari za Tanzania na kwamba linahusu uendelezaji na uboreshaji wa utendaji wa bandari.

Amesema Chama cha Mapinduzi (CCM) kisinge ruhusu serikali yake kuuza bandari kwa sababu sio sera ya CCM. “Rais Samia Suluhu Hassan ambaye ndiye Mwenyekiti wa CCM kamwe asingeruhusu azimio la kuuza bandari na sisi kama wabunge tusinge pokea azimio hilo,” amesema.

Prof. Mkumbo amesema kumekuwa na hofu ambazo kama wabunge wanapaswa kuzipokea, kuzielewa na kuzishughulikia kwa kuzingatia matakwa ya wananchi.

Advertisement

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *