PSG yahamia kwa Gavi

Wababe wa soka la Ufaransa Paris Saint-Germain (PSG) wanafikiria kuwasilisha ombi la uhamisho wa kiungo wa FC Barcelona Pablo Martín Páez Gavira maarufu Gavi majira ya kiangazi

PSG kwa muda mrefu wamekuwa wakivutiwa na kinda huyo mwenye umri wa miaka 19 ambaye jarida The Athletic la nchini Hispania limemtaja kwenye orodha fupi ya wachezaji wanaolengwa kwenye dirisha la usajili la majira ya kiangazi.

Ikiwa utakamilika Uhamisho huo utamfanya Gavi kuungana tena na kocha wake wa zamani Luis Enrique, ambaye alicheza kwa mara ya kwanza walikutana katika klabu ya Barca akiwa na umri wa miaka 17.

Advertisement

Barcelona hawana nia ya kumuuza kiungo huyo kutoka katika academy yao ya La Masia lakini kutokana na hali mbaya ya kifedha, klabu hiyo inaweza kulazimika kumwachia endapo watapata ofa nzuri.

/* */