PSSSF yafafanua lifti kuanguka Millennium Tower

MFUKO wa Hifadhi ya Jamii wa Watumishi wa Umma (PSSSF) umesema utachukua jukumu la kurekebisha hitilafu zilizojitokeza katika jengo la Millennium Tower 2, lililopo Kijitonyama Dar es Salaam baada ya ‘Lifti’ kuanguka ikiwa na watu wanaosadikia kuwa ni saba leo.

Taarifa ya PSSSF imesema kuwa kama wamiliki wa jengo watashirikiana na msimamizi wa jengo Ms. Prolaty Ltd ili kurejesha huduma zingine kama ilivyo awali.

PSSSF wameeleza kuwa kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi wanaendelea kuchunguza chanzo cha hitilafu hiyo.

Mapema leo mchana watu saba walijeruhia na kupelekwa Hospitali ya Kairuki kupata matibabu baada ya lifti kuporomoka kutoka ghorofa ya 10 katika jingo hilo.

 

 

 

Habari Zifananazo

Back to top button