Putin afuta deni $23B Afrika

RAIS wa Urusi, Vladimir Putin amesema taifa hilo imefuta na kusamehe madeni ya mataifa ya Afrika yenye thamani ya Dola bilioni 23.

Putin amefuta madeni hayo kwa kauli yake aliyoitoa jana Julai 28, 2023 katika mkutano wa pili wa kilele wa Urusi na Afrika unaofanyika mjini Saint Petersburg nchini humo.

Putin alibainisha kuwa uhusiano wa Urusi kwa Afrika unazidi kukua, jambo ambalo linadhihirika katika mipango ya kuongeza uwepo wa kidiplomasia barani humo.

“Hii ni hatua ya kweli ya kuzidisha kazi kwa kiasi kikubwa na nchi za Afrika katika nyanja za kisiasa, biashara, kibinadamu, kiutamaduni na utalii.” alisisitiza.

Moscow pia inaunga mkono uwakilishi zaidi wa nchi za kiafrika katika Baraza la Usalama na miundo mingine ya Umoja wa Mataifa,” alisema.

“Jukumu la kisiasa na kiuchumi la Afrika linakua kwa kasi, bara linakuwa kituo kipya cha mamlaka, ambacho kila mtu atalazimika kuzingatia,” aliongeza.

Putin alitoa mfano wa mpango wa amani wa Afrika kwa Ukraine kama mfano wa kuongezeka kwa jukumu la kisiasa la bara hilo.

“Hii yenyewe inasema mengi, kwa sababu hapo awali misheni zozote za upatanishi zilihodhiwa pekee na nchi zilizo na kile kinachoitwa demokrasia iliyoendelea,” alisema Putin.

Habari Zifananazo

3 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button