Putin atishia kutwaa maeneo mengine Ukraine

URUSI: Rais wa Urusi Vladimir Putin ametishia kuwa anaweza kuamuru wanajeshi wake kunyakua ardhi zaidi nchini Ukraine ili kulinda eneo linalopakana na Urusi.

Katika baadhi ya matamshi yake ya kina kuhusu vita vilivyodumu kwa miezi kadhaa, kiongozi huyo wa Urusi pia alidai kwamba vikosi vya Ukraine vimepata hasara ya “kubwa” katika mashambulizi mapya, na akasema hakuwa anafikiria uhamasishaji mpya wa askari, kama Warusi wengi wanadhania. 

Lakini hakuondoa mwito mwingine wa askari baadaye. Na alikariri madai ya Urusi kwamba Ukraine ilihusika na kulipua bwawa la Mto Dnieper ambalo lilisababisha mafuriko makubwa pande zote mbili za mstari wa mbele wiki iliyopita.

Maoni ya Putin katika mkutano wa wazi na wanahabari wa kijeshi na wanablogu yalifuatia madai ya Kyiv kwamba wanajeshi wa Ukraine waliteka vijiji vichache katika hatua za awali za mashambulizi hayo walipokuwa wakitafuta kuwaondoa wanajeshi wa Urusi kutoka mikoa minne ya Ukraine Kremlin iliyonyakua kinyume cha sheria msimu uliopita. Mkutano huo uliochukua zaidi ya saa mbili umekuja baada ya mashambulizi ya makombora ya Urusi katikati mwa Ukraine kuwaua takriban watu 11.

Putin alisema mashambulizi ya Ukraine hayajafaulu. Alidai kuwa Ukraine ilipoteza vifaru 160 na zaidi ya magari 360 ya kivita, huku Urusi ikipoteza vifaru 54 tangu mashambulizi mapya yaanze. Madai hayo hayakuweza kuthibitishwa mara moja. Maafisa wa Kiukreni kwa kawaida hawatoi maoni yoyote juu ya hasara.

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button