PUTIN: Uasi wa Wagner ni uhaini

Rais wa Urusi Vladimir Putin anasema “maasi ya kutumia silaha” ya kikosi cha mamluki cha Wagner Group ni uhaini, na kwamba yeyote ambaye amechukua silaha dhidi ya jeshi la Urusi ataadhibiwa.

Akizungumza wakati wa hotuba ya dharura iliyotangazwa kwenye televisheni, Putin amesema atafanya kila njia kuilinda Urusi, na kwamba “hatua madhubuti” itachukuliwa ili kuleta utulivu huko Rostov-on-Don, mji wa kusini ambapo Mkuu wa Wagner Yevgeny Prigozhin alisema kuwa vikosi vyake vimechukua udhibiti wa mitambo yote ya kijeshi.

Advertisement
6 comments

Comments are closed.