Pwani, Dar, kuwa na upungufu wa maji

Dawasa waboresha mifumo ya maji Kisarawe

DAR ES SALAAM: Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) imetoa taarifa kwa Wateja wake na Wananchi wanaohudumiwa na mtambo wa kuzalisha maji Ruvu Chini kuwa, kutakuwa na upungufu wa huduma ya maji kuanzia leo Jumanne Machi 5, 2024.

Taarifa ya Dawasa kwa wateja wake inasema kuwa upungufu huo wa maji unatokana na maboresho ya msingi katika mtambo wa kuzalisha maji Ruvu Chini hadi Alhamis March 7,2024.

Taarifa hiyo ya Dawasa inasema maeneo yote yanayohudumiwa na vituo vya Bagamoyo, Mapinga, MaMabwepande, Bunju, Tegeta, Kunduchi, Mbweni, Boko, Salasala, Goba, Mivumoni, Madale, Goba, Kawe, Lugalo, Makongo, Chuo Kikuu UDSM, Mwenge, Chuo Kikuu Ardhi, Kijitonyama, Mikocheni, Msasani, Oysterbay, Masaki, Mwananyamala, Kinondoni, Magomeni, Kigogo, Chang’ombe, Keko, Kurasini, Kigamboni, Airport, Kiwalani, Buguruni, Vingunguti, Ilala na Katikati ya Jiji.

Advertisement

“DAWASA inawashauri Wananchi kuhifadhi maji ya kutosha katika kipindi hiki,” imesema.

/* */