Qatar yatarajia mapatano zaidi Israel, Hamas

MAJED Al-Ansari, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Qatar, ameiambia amesema nchi hiyo inatarajia kuona mapatano kati ya Israel na Hamas yakiendelezwa zaidi.

Tumepata uthibitisho kutoka kwa Hamas kwamba mateka wengine 20 wataachiliwa huru siku mbili zijazo, na kwa upande wa Palestina ambayo itamaanisha kutoka jela za Israel …

Wapalestina 65 wataachiliwa kutoka magereza ya Israel,” al-Ansari alisema.

“Huu ni wakati wa matumaini kwetu kwamba tunaweza kuendeleza kasi hiyo ya kuongeza idadi ya mateka wanaoachiliwa lakini pia kuandaa mazingira ya makubaliano endelevu zaidi ya mazungumzo yanayofanyika.

“Tulianza mchakato huu wa upatanishi huko Doha mara tu baada ya Oktoba 7 na tulitoa michango mingi. Tulihama kutoka mahali ambapo hapakuwa na nafasi ya upatanishi,”

Habari Zifananazo

Back to top button