Radi yaua 2 familia moja

Radi yaua 2 familia moja

WATU wawili wa familia moja wamefariki Dunia baada ya kupigwa na radi katika Kata ya Msimbati, mkoani Mtwara.

Akizungumza leo mkoani Mtwara, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Nicodemus Katembo, amesema tukio hilo lilitokea Machi 19, mwaka huu saa 4 asubuhi.

Kamanda huyo aliwataja marehemu hao kuwa ni Shani Salum (53) na Nangomwa Salum (58), wote wakiwa wakazi wa kijiji hicho ambao wamefariki Bahari ya Hindi wakiwa wanatekeleza shughuli zao za uvuvi wa samaki.

Advertisement

Amesema siku ya tukio hilo majira ya asubuhi, Shani na Nangomwa walienda katika shughuli zao za uvuvi kwenye bahari hiyo wakiwa na mtumbwi,  ndipo mvua kubwa ilianza kunyesha ndipo ghafla walipigwa na Radi.