Radi yauwa watu tisa Australia

QUEENSLAND, Australia: TAKRIBAN watu tisa, akiwemo mtoto wa umri wa miaka tisa, wameuawa nchini Australia huku mvua kubwa ya radi ikipiga eneo la mashariki mwa nchi hiyo wakati wa sikukuu ya Krismasi.

Mvua kubwa ya mawe pamoja na upepo mkali yalikumba majimbo ya Victoria, New South Wales na Queensland siku ya Krismasi na Boxing Day.

Taarifa kutoka nchini Australia zinaeleza pia mtu mmoja amepotea kufuatia dhoruba iliyosababisha kukatika kwa umeme.

Upepo mkali uliezua paa na kuangusha miti katika baadhi ya maeneo yaliyoathirika zaidi ya Queensland, ambapo mwanamke mwenye umri wa miaka 59 alikufa baada ya kuangukiwa na mti katika jiji la Gold Coast Jumatatu.

Habari Zifananazo

7 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button