RAHA zinazidi kuongezeka kwa Yanga ya Dar es Salaam.
–
Yanga tayari imetetea ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, imeingia fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika na leo imeingia fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC), baada ya kuifunga Singida Big Star bao 1-0 mchezo wa Nusu Fainali Uwanja wa Liti mjini Singida.
–
Bao hilo pekee katika mchezo huo lililofungwa na Fiston Mayele muda mfupi baada ya kuingia akitokea benchi, maana yake Yanga itakwenda kukutana na Azam FC katika mchezo wa fainali. Yanga ni bingwa mtetezi wa kombe hilo.
Comments are closed.