Raia wajipanga kuokoa Precision Air kwa kamba

Wananchi wakisaidia kuokoa ndege ya Precision Air

RAIA kadhaa wamejipanga msitari kusaidia kuinusuru ndege ya shirika la ndege la precision air isizame majini baada ya kuanguka katika ziwa victoria sekunde chache kabla ya kutua katika uwanja wa ndege wa Bukoba.

Ingawa vyombo vya uokozi vinatumia boti na winchi kuvuta ndege hiyo iliyopata ajali majira ya saa 2:35 asubuhi, wananchi wameungana kusaidia kuvuta ndege hiyo kwa kamba.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Kagera, William Mwampaghale amethibitisha mapema kuwa abiria waliokuwa katika ndege hiyo wameokolewa.

Advertisement

Shirika la Ndege la Precision halijaweza kutoa taarifa yoyote hadi sasa.