Raila awasilisha ombi kwa mtandao kupinga matokeo ya urais

Raila Odinga

Timu ya wanasheria wa mgombea urais wa Azimio Raila Odinga tayari imewasilisha nakala ya kielektroniki ya ombi la kupinga ushindi wa Rais Mteule William Ruto.

Timu ya mawakili, kwa mujibu wa sheria, ina hadi saa 8 mchana wa leo kuwasilisha pingamizi lao dhidi ya ushindi wa Ruto.

Seneta mteule wa Makueni Dan Maanzo, mmoja wa mawakili katika timu ya wanasheria, amethibitisha kuwa kesi hiyo ilikuwa imewasilishwa rasmi kwa njia ya kielektroniki Jumatatu asubuhi katika Mahakama ya Juu.

Advertisement