Rais Dk Mwinyi akubali ombi waziri wa utalii kujiuzulu

RAIS wa Zanzibar ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Ally Mwinyi amekubali ombi la kujiuzulu kwa Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale, Simai Mohammed Said.

Taarifa iliyotolewa leo na kusainiwa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Zena Ahmed Said imeeleza kuwa kukubali kwa Rais Dk Mwinyi ni kwa mujibu wa kifungu cha 129 cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo kukubali kwa Dk Mwinyi kunaanza leo, hivyo kuanzia taarifa hiyo ilivyotolewa, Simai Mohammed Said sio waziri tena wa wizara hiyo.

Katika video fupi iliyotolewa na kiongozi huyo usiku wa kuamkia leo, alioneka akitoa uamuzi wake wa kutaka kujiuzulu nafasi hiyo na kueleza kuwa amemuandika barua rasmi Rais Dk Mwinyi.

Habari Zifananazo

Back to top button