Samia atuma salamu za pole kifo cha Balozi

RAIS wa Tanzania, Dk Samia Suluhu Hassan amepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha Balozi Celestine Mushi, Balozi wa Tanzania nchini Austria na Mwakilishi wa Kudumu wa Mashirika ya Kimataifa, Vienna.

Taarifa ya Rais Dk Samia imeeleza kuwa Taifa limeondokewa na mwanadiplomasia mahiri na mtumishi makini wa umma.

Akitoa taarifa za kifo hicho, Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Siriel Mchembe amesema kuwa balozi huyo alifariki katika ajali iliyotokea eneo la Mkata wilayani Handeni mkoani Tanga. Amesema alikuwa akiendesha gari akitokea Dar es Salaam kuelekea Moshi mkoani Kilimanjaro.

Mushy aliteuliwa na Rais Samia Suluhu kuwa Balozi wa Tanzania nchini Austria mnamo Januari mwaka huu na Mei 5, 2022 akawasilisha Hati za Utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Austria, Alexander Van der Bellen.

Mchembe amesema kuwa ajali hiyo imetokea juzi Jumanne usiku ambapo mwili wa balozi huyo umekutwa ukiwa umeungua.

“Mwili wa balozi tuliuchukua eneo la ajali usiku na tumeuleta Hospitali yetu ya Wilaya. Ndugu zake wapo njiani wakitokea Mbezi Dar es Salaam wanakuja kuuchukua,” amesema Mchembe.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x