RAIS wa Tanzania, Dk Samia Suluhu Hassan amekusudia kufanya mabadiliko ya baadhi ya viongozi wa Serikali ili kuachana na viongozi ambao wanashindwa kuendana na kasi yake.
Dk Samia amesema hayo leo katika Mkutano wa 10 wa chama hicho unaofanyika Dodoma ambapo amesema kuwa wanasafari ya miaka mitatu kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu mwaka 2025, ili wananchi wawe mashuhuda wa yanayofanywa.
“Kubwa zaidi tunapokwenda kwa wananchi, ni wananchi wenyewe wanayosema serikali waliyofanya kwao, tofauti na utamaduni tuliokuwa nao nyuma, kwamba tunapokwenda kwa wananchi serikali ndio tunawaambiwa tumewafanyia, wakati mwingine wanashangaa hiki kimefanyika wapi,”amesema Dk Samia.
Amesema mabadiliko hayo yatatoa nafasi kwa wananchi kuona na kutoa tathmini ya yaliyofanyika na wenyewe kuwa mashuhuda wa kila kinachofanyika.