RAIS Dk Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuzindua mradi wa maji wa Tegeta A na Mshikamano Desemba 15, 2022
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makala leo Desemba 2,20220 alipotembelea miradi hiyo ambayo imekamilika kwa asilimia 96 na kuzungumza na wananchi.
Miradi hiyo hadi kukamilika kwake itagharimu shilingi bilioni 75.
Mradi wa Tegeta A utawanufaisha wakazi wa Kata ya Mbweni, Goba, Makongo, Wazo, Bunju, Mabwepande na Mapinga Bagamoyo wakati mradi wa Mshikamano utanufaisha wakazi wa Kibamba, Mbezi, Msakuzi, Madale na Mpiji Magoe.
Nipende kumshukuru sana Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa msukumo wake wa kuridhia kiasi cha zaidi ya bilioni 75 kukamilisha miradi hii mkubwa, sehemu ya fedha hii zimetoka katika fedha za Uviko 19.” Amesema
Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam, Amos Makala na kuongeza
“Jimbo la Kibamba mwaka 2010 tulilipoteza kutokana na ukosefu wa maji, kwenye kampeni ukipita mzozo ulikua ni maji, suala hilo sasa limekwisha.”Amesema
Aidha, ameitaka Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (Dawasa), kuharakisha unganishiaji maji kwa wananchi ili ifikapo Desemba 15 maji yawe yamewafikia idadi kubwa ya wananchi.
“Dawasa zingatieni ‘deadline’, msifanywe nisutwe na watu huko mitandaoni, sio inafika tarehe wananchi maji hayajawafikia wakati nipo hapa kifua mbele nawatangazia watapata maji tarehe 15, watu wanarekodi hapa, wengine wanaviswaswadu lakini wanarekodi ikifika tarehe 15 wanisute, staki kusutwa.” Amesema Makala, kauli iliyofanywa umati wa wananchi kuangua kicheko.
Kwa upande wa Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasa, Cyprian Luhemeja amewataka wananchi wa maeneo yote ya miradi hiyo kujitokeza kwa wingi kwenye Ofisi za Dawasa kujiandikisha ili waweze kufungiwa maji.
“Tutatoa mkopo wananchi ili waunganishiwe maji, tutawaunganishia na watalipia kidogo kidogo, kupitia bili zao za maji.” Amesema Luhemeja
Nae, Diwani wa Wazo, David Manyama kwa akizungumza kwa niaba ya wananchi alimshukuru Rais Samia kuwezesha kukamilika kwa mradi huo ndani ya miaka miwili.