Rais FIFA aipa tano Morocco

Rais wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) Gianni Infantino amepongeza matokeo ya timu za Afrika katika michuano ya Kombe la Dunia la FIFA 2022 nchini Qatar.

Pongezi hizo ni baada ya Morocco kuweka historia ya kufuzu kwa nusu fainali ya michuano hiyo ikiwa timu ya kwanza ya taifa kutokea katika bara la Afrika kuwahi kuvuka hatua ya robo fainali.

“Nadhani Morocco ilicheza vizuri sana – walikuwa na mafanikio makubwa na walifanya kazi vizuri sana,” rais wa FIFA amesema.

“Walicheza kwa hamu kubwa, dhamira na ubora usiopingika.

Kufika fainali za Kombe la Dunia hakuwezi kufanyika kwa bahati.

Ni matokeo ya juhudi za muda mrefu, uwekezaji wa shirikisho la soka la Morocco, wafanyakazi wote wa kiufundi, na kocha kijana wa Morocco ambaye pia amekuwa katika soka ya klabu nchini.

“ameongeza.

Habari Zifananazo

Back to top button