RAIS wa Hungary, Katalin Novak anatarajiwa kuwasili leo na kufanya ziara yake nchini Tanzania kuanzia leo Julai 17 mpaka Julai 20 ,2023. Ziara hiyo ni matokeo ya jitihada ya Rais samia suluhu hassan za kuimarisha uhusiano wa kidplomasia na mataifa mengine.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk Stergomena Tax amesema kufanyika kwa ziara hiyo ni vipaumbele vya Rais Samia katika kuimarisha uhusiano wa kimataifa na kikanda.
Kamishna wa Kitengo cha Fedha za Nje kutoka Wizara ya Fedha, Rished Bade amesema katika ziara hiyo na Rais Katalini watajadili juu ya uwekezaji wa kilimo, utangazaji na uzalishaji wa bidhaa mbalimbali ili kuendelea kuimarisha uhusiano.
Mkurugenzi wa Kitengo cha Habari Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mindi Kusiga amesema ziara hiyo imekuja kutokana na sera mpya nchini Hungary Kwa nchi za Afrika inayolenga Kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi ambao ulianza kutekelezwa na Taifa hilo miaka michache iliyopita.