Rais Kagame, Mwenyekiti Star Times wateta

RAIS Paul Kagame wa Rwanda na Mwenyekiti wa Kampunini za Star Times wamekutana na kufanya mazungumz.

Taarifa iliyotolewa na Star Times imeeleza kuwa katika mazungumzo hayo hivi karibuni, Kagame alisema anathamini bidhaa na teknolojia bora inayotumiwa na StarTimes.

“Rais huyo alisema amefurahi kukutana tena na Mwanzilishi na Mwenyekiti huyo wa StarTimes Group, Pang XinXing,” imesema taarifa hiyo.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa Rais Kagame amesisitiza kuwa, serikali iko tayari kuipa ushirikiano wa dhati kampuni ya StarTimes katika maendeleo ya biashara nchini Rwanda.

“Kwa upande wake, Pang alimshukuru Rais Kagame na serikali yake kwa msaada na ushirikiano wake kwa StarTimes huku pia, akitambulisha maendeleo ya StarTimes Group na StarTimes nchini Rwanda.

“Alisema hivi karibuni kampuni hiyo ilizindua televisheni ya StarTime Ndani ya Dijiti katika Soko la Rwanda ikiwa ndani na teknolojia ya kisasa ya R&D yenye ubora na faida maradufu,” imesema taarifa hiyo ikimkariri Mwenyekiti huyo.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka StarTimes Dar es Salaam, katika miezi sita ya mwanzo wa mwaka ujao, StarTimes itazindua tena runinga mahiri zenye teknolojia mpya iliyojengewa ndani ili kuwapa watu wa Rwanda uzoefu bora wa TV za kidijiti.

“StarTimes iko tayari kusaidia kuharakisha utangazaji wa TV za kidijiti na kutoa mchango mkubwa kukuza maendeleo ya TV za kidijiti nchini Rwanda,” alisema mwenyekiti huyo.

Mkutano huo baina ya Kagame na Pang XinXing uliwashirikisha pia Waziri wa Tehama na Ubunifu, Ingabire Paula;  Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa RDB, Nelly Mukazayire; Mkurugenzi Mtendaji wa StarTimes Rwanda, Wang Fan na Meneja Mkuu wa kampuni ya StarTimes Media, Meng Li.

Mwaka 2007 baada ya juhudi nyingi, StarTimes ilipata leseni ya uendeshaji wa TV ya kidijiti iliyotolewa na Serikali ya Rwanda, ambayo pia ni leseni ya kwanza ya uendeshaji ambayo StarTimes ilipata barani Afrika.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
3 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Mtumwa Said Sandal
Mtumwa Said Sandal
4 months ago

Chat to Live Support

MAPINDUZI.PNG
Julia
Julia
4 months ago

Working part-time and making an extra $15,000 or more online is a simple and quick method to gain money. I earned $17,000 in the previous month by working in my spare time, and I am really happy now as a result of this job.
.
.
Detail Here—————————————>>>  http://Www.OnlineCash1.Com

Zambia Revenue Authority
Zambia Revenue Authority
4 months ago

Zambia Revenue Authority

MAPINDUZII.PNG
Back to top button
3
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x