Kikwete aitaka Dawasa kuchochea maendeleo 

RAIS Mstaafu wa awamu ya nne, Dk. Jakaya  Kikwete, ameitaka Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA)  kuchochea maendeleo katika sekta ya uwekezaji na kuongeza kasi ya usimamizi wa vyanzo vya maji ili kuhakikisha rasilimali hiyo muhimu inanufaisha kizazi cha sasa na kijacho.

Ameyasema hayo mjini Kibaha, mkoani Pwani  alipotembelea banda la DAWASA katika Maonyesho ya tatu ya Uwekezaji na Biashara yanayoendelea mkoani hapo.

“Ninawapongeza kwa kazi nzuri mnayoifanya na ninawasihi muendelee kutoa huduma nzuri kwa wananchi, hususani utunzaji wa vyanzo vya maji ili maji yapatikane ya kutosha kuweza kuchochea kasi ya uwekezaji mkoa wa Pwani” amesema Dk.
Advertisement

Kikwete

Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu  DAWASA, Mhandisi Luhemeja amesema, kwa sasa Mamlaka inahamia kwenye mfumo wa kisasa zaidi wa kuboresha miundombinu ya majitaka.
“Tunabadilisha mfumo wa majitaka na kwenda kwenye mfumo wa kisasa zaidi ambao utapunguza gharama za uendeshaji na tutaanza na mkoa wa Pwani,” amesema.
“ Pia nawasihi wananchi kufuatilia matumizi yao ya maji ili kuondoka malalamiko ya ankara kubwa za maji na waendelee kutumia maji ya DAWASA kwani yana viwango vya hali ya juu,” amesema Mhandisi Luhemeja.
Akizungumzia mipango mikakati ya Mamlaka, Mhandisi Luhemeja amesema wamejipanga kwa mwaka wa fedha 2023/2024 kujenga matenki 23 maeneo mengi ya Dar es salaam ili kurahisisha upatikanaji wa maji kwa wananchi.
Maonesho ya Uwekezaji na Biashara mkoani Pwani yamezinduliwa Oktoba 6, na yanatarajiwa kufungwa Oktoba 10, mwaka huu yakibeba kauli mbiu “ Pwani sehemu sahihi kwa uwekezaji ,kwa pamoja tujenge viwanda kwa ajira endelevu”
Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *