RAIS mteule wa Libeŕia, Joseph Boakai, ambaye alimshinda Rais George Weah amesema utawala wake utaangalia kwa makini maafikiano ya uchimbaji madini ili kuhakikisha yananufaisha nchi hiyo.
–
“Hatua ya kwanza ya kuikomboa Libeŕia ni kuichukua kutoka kwa watu hawa. Imeokolewa. Jambo linalofuata ni kushughulikia masuala ambayo yanatanda katika nchi hii,” Boakai alisema, akitoa mfano wa ŕushwa na ukosefu wa huduma za msingi.
–
Boakai alisema eneo muhimu ambalo Waliberia hawajanufaika nalo ni sekta ya madini, licha ya kuwa na akiba ya madini nchini Libeŕia, ikiwa ni pamoja na almasi, dhahabu, chuma na mbao.
–
Alipoulizwa kama hii itajumuisha kupitia upya mikataba ya uchimbaji madini, Boakai alisema mapitio yatafuatiliwa iwapo itathibitishwa.
–
Boakai alimshinda Wear katika duru ya pili ya uchaguzi wa Rais wa Novemba 14, 2023, ambapo mpinzania wake huyo alikubali kushindwa na kumpongeza.


1 comments