RAIS wa Malawi, Lazarus Chakwera ameomba msaada kwa mashirika ya misaada ya kimataifa kufuatiwa uharibifu wa makazi ya watu uliotokana na kimbunga freddy kilichouwa watu 225.
Akizungumza jana jioni katika mji Mkuu, Blantyre Rais Chakwera amesema janga hilo limerudisha nyuma maendeleo ya watu kwa kiasi kikubwa na kuziomba Jumuiya za Kimataifa kuwapa misaada mbalimbali ya chakula, mavazi na malazi.
“Malawi iko katika hali ya maafa. Kile kimbunga Freddy amefanya, ni kuturudisha nyuma hata tulipokuwa tunajaribu kujenga upya, kwa sababu ya majanga yaliyopita. Na ninaomba jumuiya ya kimataifa ituangalie kwa upendeleo kama huo. tunahitaji msaada”.alisema Chakwera.
Ilikuwa ni mara ya pili ndani ya wiki tatu kwa nchi hiyo kukumbwa na kimbunga Freddy ambacho pia kiliathiri nchi jirani ya Msumbiji.
Watu wengi waliangamia katika maporomoko ya ardhi yaliyosomba nyumba dhaifu zilizojengwa kwenye miteremko.