RAIS wa zamani wa Ivory Coast, Henri Konan Bedie amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 89.
Bedie alikuwa rais wa pili wa Ivory Coast baada ya uhuru kutoka kwa Ufaransa mwaka 1960. Alitawala kuanzia 1993 hadi mdororo wa kiuchumi na madai ya ufisadi yalisababisha kuondolewa kwake katika mapinduzi ya kijeshi miaka sita baadaye.
Bedie alifariki jana katika Hospitali ya Polyclinique Internationale Sainte Anne-Marie, hospitali ya Abidjan, mji mkuu wa kibiashara wa Ivory Coast na mji mkubwa zaidi, chama chake kilitoa taarifa kwa Shirika la Habari la Agence France-Presse.
Kifo cha kiongozi wa chama cha Democratic Party of Ivory Coast-African Democratic Rally (PDCI-RDA) pia kilithibitishwa kwa shirika la habari la Reuters na jamaa, lakini sababu haikujulikana mara moja.
Kulingana na ripoti za ndani, rais huyo wa zamani alisafirishwa kwa ndege kutoka mji alikozaliwa wa Daoukro, kilomita 230 kaskazini mwa Abidjan, baada ya kuugua siku ya jana.