Rais mstaafu Mauritania akana matumizi mabaya ya uongozi

RAIS wa zamani wa Mauritania, Mohamed Ould Abdel Aziz amekanusha mahakamani madai yote anayokabiliana nayo ya kutumia vibaya mamlaka yake na kujikusanyia mali katika utawala wake.

Aziz, ambaye alitawala Mauritania kati ya 2008 na 2019, amekutana na fedheha hizo chini ya mrithi wake na Rais wa sasa Mohamed Ould Ghazouani.

Huku upande wa mashtaka ukiwa umedai kifungo cha miaka 20, kiongozi huyo wa zamani mwenye umri wa miaka 66 alizungumza kwa muda saa moja kupinga tuhuma hizo.

Advertisement

“Tuhuma hizi zote ni za uongo, si za haki an i sehemu ya njama potofu dhidi yangu,” aliiambia. “Natuhumiwa kwa ufisadi, uko wapi ufisadi wangu? Uthibitisho wa ufisadi huu uko wapi?,” alihoji Aziz

4 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *