Rais mstaafu Tunisia jela miaka minane

RAIS wa zamani nchini Tunisia, Moncef Marzouki amehukumiwa kifungo cha miaka minane jela bila kuwepo mahakamani kwa tuhuma za kushambulia usalama wa taifa na kuchochea raia dhidi ya kila mmoja wao.

“Kufuatia taarifa za mshtakiwa huyo kwenye mitandao ya kijamii, upande wa mashtaka uliidhinisha Mahakama ya Mwanzo kumfungulia kesi ya upelelezi kwa tuhuma zinazohusiana na kupanga shambulio lililokuwa na nia ya kubadili muundo wa serikali, kuhamasisha wananchi kushambuliana kwa silaha,”

“Nakutaka kutekelezwa kwa vitendo vya mauaji na wizi”. Mohamed Zaitouneh, msemaji rasmi wa Mahakama ya Mwanzo, alisema katika taarifa yake akizungumza na Radio Mosaique.Hakukuwa na maoni yoyote kutoka kwa Marzouki kuhusiana na uamuzi uliotolewa dhidi yake.

Advertisement

Mnamo Desemba 22, 2021, mahakama ya eneo hilo ilitoa uamuzi wa awali wa kumfunga Marzouki bila kuwepo mahakamani kwa miaka minne kwa tuhuma za kushambulia usalama wa serikali. Rais huyo wa zamani alikana mashtaka hayo.